Our school

NM-AIST YAIBUKA MSHINDI TENA MAKISATU 2021,

 

Bi Lucia Petro, (katikati) mtafiti aliyeiwakilisha NM-AIST katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021, ametangazwa Mshindiwa Tatu kwa jiko alilobuni linalotumia gesi asilia (biogas) kupika, Kuoka na kuchoma vyakula mbalimbali. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa Sherehe za kilele cha Mashindano hayo amempongeza Lucia na NM-AIST Kwa Ubunifu huo.

 Kwa mara ya tatu sasa tangu MAKISATU kuanzishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuibua na kukuza Wabunifu nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kimekuwa kikitoa washindi.

Naibu Makamu Mkuu wa chuo Prof. Anthony Mshandete,  kwa niaba ya NM-AIST alimpongeza Sana Bi Lucia Kwa uwakilishi mzuri wa NM-AIST kwa mara nyingine tena na aliishukuru sana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na wadau wote Kwa kuendelea kutambua mchango wake katika kuibua na kukuza Wabunifu Kwa Maslahi Mapana ya Taifa. Lucia amepata zawadi ya 2,000,000 za kitanzania na Cheti.

Back to top