Our school

Mkurugenzi wa huduma za sheria, Wizara ya Maji, Bw.Simon Nkanyemka amewataka wananchi kuendelea kuchangia huduma za maji na kulinda miundombinu ya maji ili huduma hizo ziwe endelevu.   Bw. Simoni alitoa kauli hiyo Mei 21, 2021 wakati wa ziara ya kukagua na kufanya makabidhiano ya  mradi wa maji wa vijiji vitano wenye thamani ya bilioni 11.  Mradi huo umefadhiliwa na shirika la maendeleo la Uingireza (FCDO-UK) na kusimamiwa na serikali na  Shirika la WaterAid, kituo cha umahiri katika ufundishaji na utafiti wa miundombinu ya Maji na nishati endelevu (WISE-Futures) kilichopo katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST),  TumainiJipya pamoja na eWater.  Mradi huu umesanifiwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kuchuja maji inayoondoa uchafu wote pamoja na madini ya Floraidi, ambayo yamekuwa ni tishio kubwa kwa afya za wananchi wa maeneo ya Arusha na maeneo ya jirani na unatumia teknolojia ya malipo ya kabla ya kabla (pre-paid)  Mradi utakaohudumia wananchi wa vijiji vya Olkokola na  Lengijave pamoja na  vitongoji vya Ngaramtoni, Seuri na Ekenywa vya Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni.  Katika ziara hiyi mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Hargeney Chitukuro amesema mradi huu umeanza kunufaisha watu 23,000 katika vijiji hivyo.  Wakati huo huo, Mwenyekiti wa kijiji cha Olkokola ameishukuru serikali na wadau wa maendeleo kwa kuwaletea karibu huduma ya maji na kuomba serikali kusambaa maji katika vijiji vya jirani ambavyo havijapata maji.  Kwa mujibu  wa mkurugenzi mkaazi wa WaterAid Tanzania, Bi.Anna Mziga amesema anajivunia kukabidhi mradi huu kwa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira  (AUWSA), lengo lilikuwa ni kuwafikia wananchi wa pembezoni husaini walikuwa na changamoto ya maji Safi, mradi huu utawanufaisha  wananchi takribani 50,000 ifikapo 2030.  Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Arusha  wakati wa uanzishwaji wa mradi huu, Dr.Wilson Mahela Charles, aishukuru NM-AIST kwa kuchagua teknolojia nzuri ya uchuja wa maji hususani katika kuondoka madini ya floraidi.  Mradi huu umekabidhiwa  kwa AUWSA ukiwa Kamili asilimia 100, huku ombi kubwa  kutoka kwa wananchi likiwa urahisishwaji wa njia za malipo ili waweze kupata huduma kwa wakati.

Serikali ya ahidi Kuendelea Kutatua Changamoto za Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

Mkurugenzi wa huduma za sheria, Wizara ya Maji, Bw.Simon Nkanyemka amewataka wananchi kuendelea kuchangia huduma za maji na kulinda miundombinu ya maji ili huduma hizo ziwe endelevu.

Bw. Simoni alitoa kauli hiyo Mei 21, 2021 wakati wa ziara ya kukagua na kufanya makabidhiano ya  mradi wa maji wa vijiji vitano vilivyopo Arusha wenye thamani ya bilioni 11.  Mradi huo umefadhiliwa na shirika la maendeleo la Uingireza (FCDO-UK) na kusimamiwa na serikali ikishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo:  Shirika la WaterAid, kituo cha umahiri katika ufundishaji na utafiti wa miundombinu ya Maji na nishati endelevu (WISE-Futures) kilichopo katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST), Tumaini Jipya pamoja na eWater na unatumia teknolojia ya malipo ya kabla ya kabla (pre-paid).

Kazi kubwa ya wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST) kupitia kituo cha Umahiri katika Ufundishaji na Utafiti wa Miundombinu ya Maji na Nishati endelevu (WISE-Futures) ilikuwa kutafiti juu ya teknolojia sahihi ya kuchuja maji ili kuondoa uchafu na vimele vya magonjwa mbalimbali ikiwemo madini ya foraidi. sanjari na hayo, wataalam hawa walifanya usanifu mitambo hiyo kwa ufanisi zaidi.

Mradi huo utahudumia wananchi wa vijiji vya Olkokola,  Lengijave  na  vitongoji vya Ngaramtoni, Seuri na Ekenywa katika Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni.  Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Hargeney Chitukuro alisema mradi huu umeanza kunufaisha watu 23,000 katika vijiji hivyo.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa kijiji cha Olkokola aliishukuru serikali na wadau wa maendeleo kwa kuwaletea karibu huduma ya maji na kuomba serikali kusambaa maji katika vijiji vya jirani ambavyo havijapata maji.

Kwa mujibu  wa Mkurugenzi Mkaazi wa WaterAid Tanzania, Bi.Anna Mziga amesema anajivunia kukabidhi mradi huu kwa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira  (AUWSA), lengo lilikuwa ni kuwafikia wananchi wa pembezoni husaini walikuwa na changamoto ya maji Safi, mradi huu utawanufaisha  wananchi takribani 50,000 ifikapo 2030.

 Dr.Wilson Mahela Charles, ambaye aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Arusha  wakati wa uanzishwaji wa mradi, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa(NEC), aishukuru NM-AIST kwa kuchagua teknolojia nzuri na ya kisasa ya kuchuja maji hususani katika kuondoka madini ya floraidi ambayo yamekuwa changamoto kubwa kwa afya za wananchi wa Arusha na maeneo ya jirani. Mradi huu umekabidhiwa  kwa AUWSA ukiwa umekamilika kwa asilimia mia moja.

 

Back to top