Event Detail

  • Start Date 11/08/2025
  • Start Time 12:00 AM
  • End Date 12/10/2025
  • End Time 11:55 PM
  • Location The Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST)

UFADHILI WA SAMIA (SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+) KATIKA FANI ZA SAYANSI YA DATA, AKILI UNDE NA SAYANSI SHIRIKISHI

(DATA SCIENCE, ARTIFICIAL INTELIGENCE AND ALLIED SCIENCES)

SHAHADA YA UZAMILI, MWAKA WA FEDHA 2025/2026

A.     UTANGULIZI

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inatekeleza programu maalum ya SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP DS/AI+ inayolenga kuongeza na kukuza ujuzi wa vijana wa Kitanzania katika fani za Sayansi ya Data, Akili Unde na Sayansi Shirikishi (Data Science, Artificial Intelligence and Allied Sciences).

Wizara, kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia inapenda kutangaza fursa za ufadhili wa masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kwenye masomo ya Data Science, Artificial Intelligence, Cybersecurity, Machine Learning na maeneo kama hayo.

B.    MAENEO YA UFADHILI

Ufadhili wa SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP DS/AI+ utajumuisha:

  1. Ada ya Mafunzo.
  2. Posho ya chakula na malazi
  3. Posho ya vitabu na viandikwa
  4. Mahitaji maalum ya programu (Special Faculty Requirements)
  5. Utafiti
  6. Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu

C.    VYUO VIKUU VINAVYOLENGWA

Ufadhili utatolewa kwa waombaji wenye udahili katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Arusha au Kampasi ya Zanzibar ya India Institutes of Technology (IIT), Madras.

D.     MUDA WA UFADHILI

Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharimiwa kwa kipindi cha miaka miwili ya masomo kuanzia mwaka 2025 kulingana na programu husika walizodahiliwa.

E.     SIFA ZA WAOMBAJI WA UFADHILI

Ufadhili huu utatolewa kwa wanafunzi waliohitimu shahada ya kwanza wenye sifa zifuatazo:

  1. Awe mtanzania.
  2. Awe na sifa za kumuwezesha kuajiriwa kama Mkufunzi Msaidizi (Tutorial Assistant ) katika Taasisi za Elimu ya Juu za Umma.
  3. Muombaji wa ufadhili atatakiwa pia kuomba udahili wa kusoma shahada ya Uzamili katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela au Kampasi ya Zanzibar ya India Institutes of Technology (IIT), Madras katika masomo lengwa kama ilivyoanishwa katika kipengele A hapo juu.

F.     MASHARTI YA UFADHILI

Mwanafunzi atakayepata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:

  1.  Awe na udahili katika programu tajwa za masomo katika taasisi
  2. Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na COSTECH;
  3. Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja.
  4. Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila ya idhini ya maandishi kutoka COSTECH;
  5. Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya na zilizothibitishwa na daktari na kukubalika chuo husika;
  6. Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwenda kwa:

                                                               Mkurugenzi Mkuu,

                                                               Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia

                                          S.L.P 4302

                                                               Dar es Salaam, TANZANIA.

                                                               Barua pepe: dg@costech.or.tz

G.UTARATIBU WA KUWASILISHA MAOMBI YA UDAHILI

Maombi ya udahili yawasilishwe kupitia mfumo wa maombi wa Taasisi husika.

  1. Kwa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela maombi yawasilishwe kupitia tovuti (https://admission.nm-aist.ac.tz) na
  2. Kwa IIT Madras Kampasi ya Zanzibar maombi yawasilishwe kupitia tovuti (https://admissions.iitmz.ac.in/mtechdsai)

H.MUDA WA KUWASILISHA MAOMBI

Maombi udahili yawasilishwe kuanzia tarehe 10 Novemba 2025 hadi 10 Disemba,
2025 kwa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na tarehe
1 Novemba 2025 hadi 24 Novemba 2025 kwa IIT Madras Kampasi ya Zanzibar.
Majina ya watakaopata udahili katika taasisi hizi mbili yatawasilishwa COSTECH na
taasisi husika kwa ajili ya kufikiriwa kupata ufadhali wa masomo (Scholarship).

Imetolewa na:

                                Katibu Mkuu,

                                Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Novemba 8, 2025

                                Dodoma

 

Bofya hapa kupakua Tangazo