Event Detail

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

ORODHA YA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUPATA UFADHILI WA MASOMO
KATIKA VYUO VIKUU BORA DUNIANI KATIKA FANI ZA SAYANSI YA DATA,
AKILI UNDE, NA SAYANSI SHIRIKISHI KWA MWAKA 2025/2026 (SAMIA
SCHOLARSHIP EXTENDED FOR DATA SCIENCE, ARTIFICIAL INTELLIGENCE,
AND ALLIED SCIENCES)

 

 

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuwaarifu waombaji wa fursa za ufadhili wa masomo katika ngazi ya Shahada ya Kwanza kupitia programu ya SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED (DS/AI+) kwa mwaka wa masomo 2025/26, kuwa orodha ya majina kwa waombaji waliochaguliwa ni kama yalivyoambatanishwa kwenye tangazo hili.

Waombaji wote waliopata ufadhili huu wanatakiwa kujiunga na kambi maalum ya maarifa kwa ajili ya maandalizi ya kujiunga na vyuo vikuu bora duniani kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo ulioambatishwa na tangazo hili. Maandalizi hayo yataanza tarehe 15 Septemba 2025 katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha.

Orodha ya majina na mwongozo wa kujiunga na kambi hiyo vinapatikana kwenye Tovuti rasmi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://www.moe.go.tz), Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (https://www.costech.or.tz) na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (https://nm-aist.ac.tz).

 

ANGALIZO:

Waombaji waliokosa ufadhili huu wanahimizwa kuomba ufadhili wa Samia (kwa vyuo vya ndani) kama ilivyotangazwa awali.

 

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Julai 9, 2025
DODOMA

DOCUMENTS