Event Detail

  • Start Date 07/12/2025
  • Start Time 12:00 AM
  • End Date 08/08/2025
  • End Time 12:00 AM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

TANGAZO LA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KATIKA VYUO VIKUU BORA
DUNIANI KATIKA FANI ZA SAYANSI YA DATA, AKILI UNDE NA SAYANSI
SHIRIKISHI KWA MWAKA 2025/2026 (SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DATA
SCIENCE/ARTIFICIAL INTELLIGENCE +)

 

1.UTANGULIZI

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza fursa za ufadhili wa masomo katika ngazi ya Shahada ya Kwanza na Shahada ya Umahiri kupitia programu ya SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+ (SSE- DS/AI+) kwa mwaka wa masomo 2025/26.
  2. Programu ya SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+ itatoa ufadhili kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao ya awali na wanaotaka kujiendeleza kitaaluma katika fani za “Data Science, Artificial Intelligence, Cybersecurity, Machine learning na Allied Sciences”.
  3. Ufadhili huu ni wa asilimia mia moja (100%) ukijumuisha ada ya masomo, udahili wa chuo na usajili wa kozi, gharama za utafiti, posho ya kujikimu, bima ya afya, usafiri, makazi na gharama za kujifunza lugha.

2.UFADHILI WA SHAHADA YA KWANZA

  1. Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita ambao majina yao yameorodheshwa kwenye Tovuti rasmi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://www.moe.go.tz) Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) (https://www.costech.or.tz) au Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) [https://nm-aist.ac.tz] .
  2. Mwombaji wa ufadhili awe na sifa zifuatazo:
    • Awe Mtanzania;
    • Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha sita mwaka 2025 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za PCM, PGM au PMC; na ambaye jina lake limeorodheshwa kwenye tovuti rasmi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, COSTECH, au NM-AIST.
  3. Mafunzo ya shahada ya kwanza yatatanguliwa na kambi ya mafunzo ya maandalizi (Bootcamp) ambayo yatafanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya
    Nelson Mandela, iliyopo Tengeru-Arusha kwa kipindi cha miezi kumi (10).
  4. Ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+ ni wa muda wa miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.
  5. Maombi ya SSE- DS/AI+ kwa shahada ya kwanza yatafanyika kwa mwanafunzi na mzazi/mlezi kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa, na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa njia ya barua pepe ps@moe.go.tz. (Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 8 Agosti, 2025.)

3.UFADHILI WA SHAHADA YA UMAHIRI

  1. Ufadhili huu utatolewa kwa wanafunzi waliohitimu shahada ya kwanza wenye sifa zifuatazo:
    • Awe Mtanzania.
    • Awe na udahili wa kusoma shahada ya Umahiri katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) au IIT Madras Zanzibar kozi za Data Science, Artificial Intelligence, Cybersecurity Machine Learning na Allied Sciences.
    • Awe na umri usiozidi miaka 35.
    • Awe na GPA isiyopungua 3.8 katika shahada ya kwanza/ Kiwango kingine kinachotambulika na Chuo husika.
  2. Wanafunzi wanufaika, watagharamiwa kwa kipindi kisichozidi miaka miwili ya masomo.
  3. Ufadhili wa masomo ya umahiri kupitia SSE- DS/AI+ utajumuisha yafuatayo;
    • Ada ya masomo;
    • Posho ya kujikimu;
    • Bima ya afya;
    • Gharama za Utafiti kwa mujibu wa miongozo ya Chuo.
    • Gharama za udahili; na
    • Usajili wa kozi
  4. Maombi ya Ufadhili kwa ajili ya shahada ya Umahiri yawasilishwe kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa njia ya barua pepe ps@moe.go.tz kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 30 Oktoba, 2025.

4. MASHARTI YA UFADHILI

Mwanafunzi atakayepata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+ atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:

  1. Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
  2. Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya kuwezesha malipo ya fedha za ufadhili.
  3. Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila idhini ya maandishi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
  4. Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, au kijamii zilizothibitishwa;
  5. Ikiwa mnufaika ataahirisha fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwa:Katibu Mkuu,
    Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
    Mji wa Serikali Eneo la Mtumba Mtaa wa Afya,
    S.L.P 10,
    40479 DODOMA, TANZANIA.
    Barua pepe: ps@moe.go.tz
  6. Wanufaika watatakiwa kuwa na ufaulu wa 3.8 kwa kila mwaka au kiwango kingine cha ubora wa juu kinachotambuliwa na chuo husika.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Julai 9, 2025
DODOMA

DOCUMENTS